Skip to main content

Viongozi wa dunia wameitaka Libya kumaliza ghasia zinazoendelea nchini humo

Viongozi wa dunia wameitaka Libya kumaliza ghasia zinazoendelea nchini humo

Uongozi wa Libya umekosolewa vikali kutokana na ghasia zinazoendelea na ukandamizaji wa waandamanaji wanaipinga serikali.

Wakizungumza kwenye mkutano wa baraza la haki za binadamu mjini Geneva hii leo mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi mbalimbali duniani wamesema usakaji na utesaji wa waandamanaji haukubaliki na wameunga mkono kusitishwa uanachama wa Libya katika baraza hilo.

Kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay amesema jumuiya ya kimataifa lazima iendelee kutoa shinikizo kwa serikali ya Libya hasa katika kuheshimu misingi ya uhuru wa raia wake na kukomesha ghasia.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)

Kamishina mkuu ameitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za kusaidia kuheshimiwa kwa haki za binadamu na mchakato wa demokrasia ambao sasa umelikumba eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.