Skip to main content

Juhudi za UNHCR za kusaidia Wakongomani walioko Burundi kurudi nchini mwao

Juhudi za UNHCR za kusaidia Wakongomani walioko Burundi kurudi nchini mwao

Juhudi za shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR pamoja na serikali za Burundi na Congo za kutaka wakimbizi wakongomani walioko Burundi kuanza kurudi nchini mwao kwa hiari zimegonga mwamba.

Wakimbizi hao wanaokadiriwa karibu 30 Elfu wamewasilisha hoja mpya ikiwa ni pamoja na kuomba uraia katika nchi ya hifadhi ya Burundi au wapelekwe kupewa hifadhi katika nchi za magharibi.

Wakuu wa HCR nchini Burundi pamoja na viongozi wa serikali ya Burundi walikuwa wiki hii katika kambi za wakimbizi wa Congo kaskazini mwa Burundi kukadiria ni wapi umefikia mpango wa kuwarejesha wakimbizi hao nchini mwao.

Muandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani KIBUGA ameambatana na ujumbe huo hadi kwenye kambi za wakimbizi na kutuandalia makala haya.