Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukoloni ni enzi iliyopitwa na wakati- KM Ban

Ukoloni ni enzi iliyopitwa na wakati- KM Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuendeleza ukoloni kwa nyakati hizi ni kupoteza wakati na ametaka kukomeshwa kwa hali hiyo.

Amesema kuna maeneo 16 ambayo hadi sasa bado hayana uhuru wa moja kwa moja kutokana na kuhodhiwa na mataifa mengine.

 

Ameyataja baadhi ya maeneo hayo ni pamoja na Bermuda, ambayo inatawaliwa na Uingereza, Guam iliyochini ya Marekani, na Sahara Magharibi ambayo inahodhiwa na Hispania