Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ivory Coast inaendelea kuzalisha wakimbizi-UNHCR

Ivory Coast inaendelea kuzalisha wakimbizi-UNHCR

Wakati mapigano yakiendelea kujiri mjini Abidjan na maeneo ya kaskazini mwa Ivory Coast, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema linawasiwasi wa kuongezeka kwa wakimbizi wa ndani katika maeno ya mipakani wanaokimbilia mashariki mwa Liberia.

Shirika hilo limesema kuwa hadi kufikia katikati ya wiki hii ilishuhudia zaidi ya watu 100 kwa siku wakivuka mpaka kwenda upande wa pili.

 

Hata hivyo taarifa zaidi zimesema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wanaovuka mipaka ambao wanakwenda kutafuta hifadhi katika maeneo mengine.

 

Shirika la umoja wa mataifa linalotoa misaada ya kiutu OCHA limesema kuwa machafuko yanayoendelea sasa yamegharimu uharibifu wa mali mbalimbali ikiwemo kuvurugika kwa sekta za afya, kilimo, elimu na kuporomoka kwa hali ya uchumi

==