Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Libya sasa inakaribia kutumbukia kwenye mapigano ya kiraia:UM

Libya sasa inakaribia kutumbukia kwenye mapigano ya kiraia:UM

Kulingana na mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na ulinzi Edward Luck amesema kuna wasiwasi mkubwa wa kuzuka machafuko ya kiraia katika siku za usoni na ametaka kuingilia kati kwa jumuiya za kimataifa.

Mjumbe huyo amesema kuendelea kusikika matukio ya kuvunja moyo kama machafuko, matumizi ya nguvu za dola kukandamiza waandamanaji, na hali ya uhasama inayoanza kuchanua sasa, ni ishara ambazo zinaashiria kukaribia kwa mapigano ya kiraia.

(SAUTI YA EDWARD LUCK)

 

Kiongozi wa Libya Muammar Al-Qadhafi ameendelea kukabiliwa na lawama kutoka kwa viongozi wa dunia wakimtaka kuzua matimzi ya nguvu kudhibiti maandamano yanayoendeshwa na wananchi waliochoshwa na utawala wake.