Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa ILO ajiunga na wengine kulaani utumiaji nguvu dhidi ya waandamanaji Libya

Mkuu wa ILO ajiunga na wengine kulaani utumiaji nguvu dhidi ya waandamanaji Libya

Kiongozi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kazi ameongeza sauti yake kwa kulaani viongozi wa Libya kwa mauaji dhidi ya wapinzani na kuashiria kwamba Libya ni mfano tosha wa hatari ya kukosekana ajira na umasikini ndani ya taifa.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la ILO Juan Somavia amewaonya viongozi wa Libya kusimamisha mara moja mauaji na kuwaacha wananchi kudhihirisha kero zao katika maadamano ya amani ikiwa ni pamoja na kuwaruhusu haki ya kueleza pamoja na haki ya mikutano.

Kiongozi huyo ameendelea kusema kwamba shabaha kubwa ya shirika lake ni hatma ya wafanyakzi wa nchini na wageni ambao wamekuwa wanakumbwa na mzozo huo.

 

 

 

 

 

Bwana Somavia ameungana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Matifa Ban Ki-moon kulaani vitendo vya kiongozi wa lybia dhidi ya waandamanaji kwa kuendesha uhalifu dhidi ya ubinadamu na kutoa wito wa kutolewa adhabu kwa wale wote wanaomwaga damu ya watu wasio na hatia.

 

 

 

 

 

 

 

Amesema kwamba sheria na kanuni za shirika la ILO zilijaaribu kuiomba Lybia kuwaacha wafanyakazi kuunda mashirika yao na hivo kujiunga na vyama vya wafanyakazi wanavyovichagua ,lakini watu waliojaribu kufanya juhudi hizo , haki yao ilivunjwa kwa utumiaji wa hatua za nguvu ikiwemo kufanyishwa kazi za nguvu.

 

 

 

 

 

 

 

Bwana Somavia amesema ni wakati wananchi kunufaika na juhudi za maendeleo kwa kuwapa hususan vijana kama matunda ya maendeleo na uheshishwaji wa haki za wafayankazi.Wakati hilo litawezekana, basi Shirika la ILO liko tayari kuisaidia Libya kuendeleza malengo hayo.