Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laongeza muda wa vikosi vya kulinda amani Timor-Leste

Baraza la Usalama laongeza muda wa vikosi vya kulinda amani Timor-Leste

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza alhamisi hii muhula wa kuwepo vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini Timor ya Mashariki kwa mwaka mmoja.Tume hii inayojulikana kama UNMIT itafanya kazi hadi tarehe 26 mwezi februari mwaka wa 2012.

Nchi 15 wajumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wameziita pande zote katika Timor Mashariki kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na kuanzisha mazungumzo ya kisiasa pamoja na kuimarisha amani, demokrasia na mfumo wa sheria nchini humo.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limethibitisha umuhimu wa kujenga upya na kufanya mageuzi ya polisi ya kitaifa PNTL kwa usaidizi wa tume ya umoja wa mataifa Timor Mashariki.

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Timor Mashariki akiwa pia mkuu wa tume ya UNMIT Ameerah Haq ameliambia baraza matumaini yake kuhusu hatma nzuri ya taifa ambalo limekuwa likiendelea.

Hata hivo ameonyesha wasiwasi kuhusu idadi kubwa ya visa vya uhalifu wa majumbani na mapigano mbalimbali kati ya vijana .

Tume ya Umoja wa Mataifa Timor Mashariki iliundwa mwaka wa 2006 baada ya mchafuko makubwa katika taifa hilo la kusini mashariki mwa Asia. Kabla ya hapo kulikuwa na tume nyingi za umoja wa mataifa hapo awali kabla ya taifa hilo kujipatia uhuru kutoka kwa Indonesia kwa usaidizi wa Umoja wa Mataifa katika mwaka wa 2002.