Hali ya usalama Afghanistan bado ni tete:UM

Hali ya usalama Afghanistan bado ni tete:UM

Mwanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan amesema kuwa hali ya usalama katika nchi hiyo bado ni ya kiwango cha chini ambayo imechochewa na kuondolewa madarakani kwa utawala wa Taliban mwaka 2001.

Robert Watkins amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa kuzorota kwa hali ya usalama kumekwaza majukumu ya mashirika ya utoaji misaada ya usamaria mwema ambayo yanashindwa kusambaza huduma zake.

 

Amesema kunahitajio kubwa la utoaji wa huduma za kiutu ambayo imeanguka kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.