Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM unamatumaini na machipuo mapya Tunisia

UM unamatumaini na machipuo mapya Tunisia

Ripoti iliyotolewa na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na haki za binadamu imeilezea Tunisia kama taifa linalochanua upya kutoka kwenye mfumo wa ukandamizaji na kuingia kwenye ukurasa mpya unaozingatia na kuheshimu mifumo ya haki za binadamu.

Ripoti hiyo imesema kuwa inatumai utawala mpya ulioingia madarakani hivi karibuni utaenzi machipuo hayo mapya ili kustawisha taifa hilo.

 

Imeulaumu utawala uliopita wa rais Ben Ali kwa kukandamiza uhuru wa haki za binadamu na kuwanyima fursa za kiuchumi wananchi wake.

 

Ripoti hiyo imeandaliwa na jopo la wataalamu wa haki za binadamu walioitembelea nchi hiyo hivi karibuni. Mona Rishmawi ni miongoni mwa wajumbe waliotembelea Tunisia:

(SAUTI YA MONA RISHMAWI)

 

Ripoti hiyo pia imetoa wito kuendesha kwa uchunguzi dhidi ya matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu ili wahusika wake wafikishwe kwenye mkono wa haki.