Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afisa wa ngazi ya juu jeshini DRC atupwa jela kutokana na ubakaji

Afisa wa ngazi ya juu jeshini DRC atupwa jela kutokana na ubakaji

Kiongozi wa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Congo, amepongeza na kukaribisha uamuzi wa mahakama moja ambayo imemkuta na hatia afisa wa jeshi juu ya makosa ya ubakaji na ukiukaji wa haki za binadamu.

Mahakama ya kijeshi ya Congo mapema wiki hii ilimuhukumu kifungu cha kati ya miaka 10 hadi 20, afisa huyo wa jeshi mwenye cheo cha juu  baada ya kubainika alihusika kwenye upaliliaji wa matukio ya ubakaji katika mji wa Fizi mwanzono mwa mwaka huu.

 

Hii ni mara ya kwanza kwa afisa wa ngazi za juu jeshini pamoja na maafisa wengine kupandishwa kizimbani na kuhumiwa kifungo.

 

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na matukio ya unyanyasaji wa kingono kwenye maeneo yaliyokumbwa na vita, Margot Wallström, amekaribisha hukumu hiyo akisema kuwa imefungua macho kwa kubainisha kuwa kumbe kuwawajibisha wale wanahusika kwenye unyanyasaji wa ngono ni jambo linalowezekana.