Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yasifu ufunguaji mipaka kuruhusu wakimbizi wa Libya

UNHCR yasifu ufunguaji mipaka kuruhusu wakimbizi wa Libya

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limesema limetiwa moyo na uamuzi wa serikali ya Tunisia na Misri ambazo zimetanagaza kuendelea kuacha wazi mipaka yake ili kuruhusu wakimbizi kutoka nchi jirani ya Libya kupita kwenye maeneo hayo.

Katika taarifa yake UNHCR imesema kuwa kwa kutilia uzito hali inavyoendelea kuchacha huko Libya,ni muhimu kuhakikisha usalama kwa wale wanaokimbia machafuko hayo unalindwa.

 

Alice Kariuki na taarifa kamili:

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)