Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICC yasema wananchi wa Libya ndiyo wanaoweza kuamua hatma ya haki yao

ICC yasema wananchi wa Libya ndiyo wanaoweza kuamua hatma ya haki yao

Mwendesha mashitaka wa mahakama ya kimataifa juu ya uhalifu Luis Moreno-Ocampo, amesema uamuzi wa kuona haki na usawa unatendeka nchini Libya upo mikononi mwa wananchi wenyewe.

Amesema Libya siyo muitifaki kwa mkataba wa Rome ambao unatambua kuwepo kwa mahakama hiyo hivyo uamuzi wa mwisho unasalia kwa wananchi wenyewe.

 

Mahakama hii ya kimataifa hata hivyo inaweza kuendesha kesi zake katika nchi ambazo ziliridhia mkataba wa Rome unaohalalishwa uundwaji wake. Fady Al-Abdallah ni wa mahakama hii:

(SAUTI YA FADY AL-ABDALLAH)

 

 

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa matukio yanayoendelea kujiri huko Afrika ya kaskazini na mashariki ya kati hayatabiriki na yanaongeza hali ya wasiwasi.

 

Ameelezea masikitiko yake kufuatia matukio ya kushambuliwa kwa waandamanaji huko Libya akisema kuwa vitendo hivyo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.