Skip to main content

Kuna mianya mikubwa ya ukiukwaji wa haki za binadamu Ivory Coast:UM

Kuna mianya mikubwa ya ukiukwaji wa haki za binadamu Ivory Coast:UM

Ripoti mpya iliyotolewa na kamishna wa umoja wa mataifa juu ya haki za binadamu imeainisha maeneo kadhaa ambayo yanaendelea kukwaza misingi ya haki za binadamu nchini Ivory Coast tangu nchi hiyo ifanye duru ya pili ya uchaguzi wa rais.

Katika ripoti hiyo Navi Pillay,amesema  vitendo vya mauaji, utekaji nyara ni baadhi ya taswira inayopatikana sasa nchini humo na ametaka kuchukuliwe kwa hatua za haraka kukomeshwa kwa hali hiyo na wahusika wake kuchukuliwa hatua.

Ripoti hiyo ambayo imeangazia matukio yaliyojiri hadi January 31 mwaka huu, imesema kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, na kiasi cha ya watu 300 wameuwawa kutokana na mkwamo wa kisiasa.

 

Askari ambao wanaunga mkono utawala wa rais anayedai kushindwa Laurent Gbagbo wanatuhumiwa kuendesha mauji hayo hasa katika maeneo ya Kusini na magharibi mwa Abidjan ambako ndiko iliko ngome ya kiongozi huyo