Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wasomalia 57 wafariki dunia baada ya kuzama kwenye pwani ya Yemen

Wasomalia 57 wafariki dunia baada ya kuzama kwenye pwani ya Yemen

Kiasi cha watu 57 raia wa Somalia wamerafiki dunia baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuzama maji katika pwani ya Yemen.

Watu hao ambao wengi wao walikuwa ni wakimbizi na wengine wafanya magendo walikuwa wakielekea nchini Yemen.

 

Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi UNHCR Andrej Mahecic amesema hata hivyo mtu mmoja ndiye aliyenusurika kwenye ajali hiyo, ambaye aliweza kuogelea kwa muda wa saa 23 na kufanikiwa kufika kwenye bandari ya Yemen iliyoko kwenye mji wa Bir Al:

(SAUTI YA ANDREJ MAHECIC)

  

Wakimbizi hao walikuwa wamepakia boti hilo karibu na eneo linalojulikana Bosasso kaskazini mwa Somalia.