Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Timor-Leste imeachana na enzi za vita, na kukaribisha maendeleo- Waziri Mkuu

Timor-Leste imeachana na enzi za vita, na kukaribisha maendeleo- Waziri Mkuu

Wananchi wa taifa la Timor-Leste hatimaye wameingia kwenye duru mpya ya mashikamano na maendeleo na kuiaga enzi ya machafuko na mizizo iliyokumba eneo hilo kwa miaka mingi.

Kulingana na Waziri mkuu Xanana Gusmao enzi ya uhasama na machafuko sasa imetoweka nchini humo mnamo ambapo taifa hilo linaingia kwenye mwongo wa pili likiwa na kauli mbiu isemayo " kwa heri machafuko, karibu maendeleo."

 

Akizungumza kwenye baraza la usalama, waziri mkuu huyo  ameutaka Umoja wa Mataifa na washirika wake kulisaidia taifa hilo ili kufanikisha uchaguzi wa rais na wabunge unaotazamiwa kufanyika mwaka ujao.