Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwekeza kwa wanawake ndiyo suluhu ya ukuzaji uchumi-Migiro

Kuwekeza kwa wanawake ndiyo suluhu ya ukuzaji uchumi-Migiro

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro amesema uwezekaji kwa

wanawake na watoto wa kike, ni jambo muhimu linaloweza kusukma mbele maendeleo

ya nchi na wakati huo huo ni njia mujarabu ya kuwawezesha wanawake.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano wa Kamisheni juu ya hali ya wanawake, unaofanyika New York, Migiro amesema wanawake wameendelea kuachwa nyuma kwa miaka mingi na kutolea mfano namna kundi kubwa la wanawake wanaokabiliwa na hali ya kutoa jua kusoma na kuandika.

(SAUTI YA ASHA-ROSE MIGIRO)

Amesema kuwa  robo tatu ya watu wote wasiojua kusoma na kuandika ni wanawake ambao takwimu zao zimeeendelea kusalia hali hiyo kwa zaidi ya miaka 20.