Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wa Libya wakimbia mapigano

Wahamiaji wa Libya wakimbia mapigano

Wahamiaji kutoka Libya wameanza kuvuka mipaka na baadhi yao wameripotiwa kupiga

hodi nchini Tunisia wakijaribu kusaka hifadhi kutokana na machafuko

yanayoendelea katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Kwa mujibu wa shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM wengi wa wahamiaji hao wanasadikika kuwa ni watu wenye asili ya Tunisia.

Hata hivyo shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema kuwa wahamiaji wengine kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Lebanon, Uturuk na Syria, wameanza kukimbia maeneo ya mijini karibu ni mpakani wakiomba msaada wa kurejeshwa makwao.

Afisa mmoja Jean Philippe Chauzy amesema kuwa Libya inawahamiaji wasio halali zaidi ya 1.5 wengi wao kutoka nchi za Afrika, mashariki ya kati na asia. Amesema usalama wa wahamiaji hao upo katika hali tete.

(SAUTI YA JEAN PHILIPPE CHAUZY)