Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu kuijadili Libya

Baraza la haki za binadamu kuijadili Libya

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa linakutana wiki hii kujadilia

mwenendo wa mambo huko Libya. Mkutano huo ni matokoe ya maombi yaliyowasishwa na Hungary kwa Umoja wa Ulaya na tayari umeungwa mkono na nchi wanachama 44.

Libya ni mwachama wa baraza hilo la haki binadamu, wanachama ambao unatazamiwa

kukoma mwaka 2013.

Miito imeendelea kutolewa kutoka kila pembe ya dunia kuhusiana na utawala wa Libya unavyojaribu kukandamiza maandamano hayo.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay amelaani vikali matukio ya kuwashambulia waandamanaji hao na kuonya kuwa hali hiyo inaweza kupindukia haki za binadamu.