Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama la laani matumizi ya nguvu kudhibiti maandamano Libya

Baraza la usalama la laani matumizi ya nguvu kudhibiti maandamano Libya

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limetoa wito wa kumalizwa haraka kwa

ghasia nchini Libya na kulaani hatua ya serikali ya nchi hiyo jinsi

ilivyopambana na waandamanaji wa upinzani.

Wanachama 15 wa baraza hilo wametaka wale wote waliohusika na mashambulio dhidi ya raia kuwajibika na kusisitiza haja ya kuheshimiwa uhuru wa kuandamana na kujieleza.

Aidha kwa upande mwingine baraza hilo limeelezea masikitiko yake kufuatia taarifa za kukosekana kwa huduma za matibabu kwa ajili ya kuwatibu majeruhi ambao idadi yao inazidi kuongezeka.Limeitaka Libya kutoa fursa kwa mashirika ya utoaji misaada kupewa fursa ya usambazaji huduma za kiafya

Balozi Maria Luiza Ribeiro Viotti kutoka Brazil ni rais baraza la usalama katika

kipindi hiki cha mwezi February:

(SAUTI YA MARIA LUIZA RIBEIRO VIOTTI)