Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

EC, UNEP kusaidia hifadhi ya msitu wa Mau nchini Kenya

EC, UNEP kusaidia hifadhi ya msitu wa Mau nchini Kenya

Kamishna ya Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP limeanzisha mradi wenye shabaya ya kusuma mbele misitu ya Mau iliyoko nchini Kenya kama njia mojawapo ya kupiga jeki azimio la kufikia mapinduzi ya uchumi wa kijani

Mpango huo ambao unatazamiwa kudumu hadi mwaka 2013 unakusudia kuyapa kipaumbele maeneo kadhaa ikiwemo eneo la kuwepo kwa matumizi endelevu ya rasilimali kwenye eneo hilo.

 

Kulingana na Mkurugenzi mtendaji wa UNEP Achim Steiner misitu ya Mau ni mshirika mkubwa anayeweza kufanikisha azma ya mapinduzi ya uchumi wa kijani wa serikali ya Kenya.

 

Ili kuleta uhalisi zaidi, pande zote mbili zimekubaliana kuinua kiwango cha miundo mbinu kwenye eneo hilo na kuongeza hifadhi ya rasilimali zinazopatikana kwenye misitu hiyo.