Skip to main content

UNESCO yasema lugha mama ziko hatarini kupotea

UNESCO yasema lugha mama ziko hatarini kupotea

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na utamaduni UNESCO limeonyesha wasiwasi wake kuhusiana na kuanguka kwa lugha zinazotambulika kama lugha mama, kutokana na kukua kwa mfumo mpya unakumbatia lugha mtawanyiko.

Mkuu wa shirika hilo Irina Bokova, akizungumza wakati wa kuandimisha kwa siku ya lugha mama ambayo huadhimishwa kila mwaka February 21, tangu mwaka 1999, amesema kuwa lugha nyingi mama zinakabiliwa na kitisho cha kupotea kabisa.

 

Amesema lengo la kuanzishwa siku ya lugha ya awali ama lugha mama, ni kuongeza mchango wa kudhamini na kuendeleza elimu kwa njia inayotambulika na kunyambulika.