Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwekeza kwenye mapinduzi ya uchumi wa kijani ndiyo hatua muafaka-UM

Kuwekeza kwenye mapinduzi ya uchumi wa kijani ndiyo hatua muafaka-UM

Umoja wa Mataifa katika ripoti yake iliyozinduliwa leo imetilia muhimu juu ya uwekezaji kwenye maeneo muhimu kadhaa ambayo imesema kuwa yanaweza kuleta mabadiliko makubwa na kuibua uchumi wa kijani.

Katika ripoti hiyo iliyopewa jina la kuelekea kwenye mapinduzi ya uchumi wa kijani, Umoja huo wa Mataifa umependekeza kuwepo kwa kiasi cha dola za kimarekanin trilioni 1.3 kwa ajili ya kufanikisha uwekezaji kwenye maeneo iliyoyaita nyeti. Imesema hatua hiyo itatoa msukumo wa kipekee wa kupunguza kiwango cha hewa chafu angani na wakati huo huo inaweza kutumia kama njia mujarabu ya kupunguza kiwango cha umaskini. Mary Muturi na taarifa kamili.

(SAUTI YA MARY MUTURI)

Ripoti hiyo imezianisha sekta kadhaa ambazo ni kiungo muhimu kwenye ufanikishaji wa mapinduzi ya uchumi wa kijani. Maeneo hayo ni pamoja na kilimo, ujenzi, nishati, uvuvi, misitu, utalii na usafiri. Pia imeyataja maeneo kama usimamizi wa taka na masuala ya maji kuwa ni maeneo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa.

Aidha ripoti hiyo imesisitiza kuwa mapinduzi ya uchumi wa kijani siyo tu yanakubalika zaidi kwa nchi zilizoendelea lakini pia ni njia inayoonekana kutoa majibu ya haraka kwenye kukabiliana na tatizo la umaskini