Kikao cha Kamisheni juu ya hali ya wanawake chaanza New York

22 Februari 2011

Kikao cha Kamisheni juu ya hali ya wanawake kimeanza leo mjini New York.Wawakilishi wa serikali pamoja na makundi ya kiharakati zaidi ya 1,500 wanaweka zingatia lao kwenye majadiliano kuhusu nafasi ya mwanamke na mtoto wa kike kushiriki kwenye elimu, mafunzo na maeneo ya sayansi.

Ama kitengo cha Umoja wa Mataifa ambacho kimeanzishwa kwa ajili ya kushughulia masuala ya wanawake kitazinduliwa rasmi hapo alhamisi na Mkurugenzi Mtendaji wa kitengo hicho Michelle Bachelet anatazamiwa kutoa hutuba maalumu.

 

Naibu Katibu Mkuu Asha-Rose Migiro naye atahutubia mkutano huo ambao unamalizika rasmi March 4.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter