Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kansa yaleta mzigo mpya kwa nchi maskini-WHO, IAEA

Kansa yaleta mzigo mpya kwa nchi maskini-WHO, IAEA

Mashirika ya Umoja wa mataifa yameonya kuwa ugonjwa wa kansa ambao kwa kiwango kikubwa ulisambaa zaidi katika nchi zilizoendelea sasa umepindukia na kuweka mzigo mpya kwa nchi maskini.

Katika taarifa yao ya pamoja mashirika hayo lile la afya duniani WHO na wakala wa silaha za atomiki IAEA, yamesema kansa imeongeza mzigo wa ziada kwa makundi ya watu maskini na wale walioko pembezoni, ambao tayari wanakabiliwa na hali ngumu za maisha.

 

Ripoti za mashirika hayo zinasema kuwa ugonjwa wa kansa ni moja ya magonjwa yanayoangamiza maisha ya watu duniani kote wanaofikia milini 7. 6 ambao hupoteza maisha kila mwaka na wengi wao ni kutoka katika nchi zinazoendelea.

 

Mashirika hayo yamesema yataendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kusaidia kasi ya ugonjwa huo katika nchi maskini