Navi Pillay ashutumu matumizi ya nguvu kwa waandamanaji wa Libya

22 Februari 2011

Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu Navi Pillay ameonya juu ya matumizi ya nguvu nchini Libya kujaribu kuzuia maandamano ya amani akisema kuwa hatua hiyo inaweza kupindukia haki za kibinadmu.

Ametoa wito kuwepo kwa tume huru ya kimataifa kwa ajili ya kuchunguza vitendo vya ukandamizaji vinavyowaandama waandamanaji hao.

 

Mkuu huyo amelani vikali juu ya matumizi ya nguvu kama silaha ambazo zinadaiwa kutumika kuwasambaratisha waandamanaji.

 

Ravina Shamdasani ni msemaji wa ofisi ya Kamishna ya haki za binadamu

 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter