Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haiti ipo hatarini kukumbwa na kipindupindu-WHO

Haiti ipo hatarini kukumbwa na kipindupindu-WHO

Shirika la afya dunaini WHO limeonya kuwa Haiti inakabiliwa na kitisho cha kukumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindipindu katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye msimu wa kanivol, lakini inaweza kujiepusha na balaa hilo kama itachukua hatua za haraka kuboresha mazingira ya kiafya.

Maafisa wa WHO wamesema kuwa kuna hatari wananchi wengi wakatumia vyakula vyema hali mbaya ya kiafya wakati wa sikuku hiyo ya kanival jambo ambalo litawasababishia kutumbukia kwenye maambukizi ya ugonjwa huo.

 

Uchunguzi uliofanywa na WHO unaonyesha kuwa kuna ulazima mkubwa wa kuboresha mifumo ya utoaji wa maji safi na salama ya kunywa wakati wa sherehe hizo, kama njia mojawapo ya kukabili mlipuko huo.

 

Fadella Chaib ni msemaji wa WHO

(SAUTI YA FADELA CHAIB)