Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Marekani yaipinga azimio la kuishutumu Israel

Marekani yaipinga azimio la kuishutumu Israel

Marekani imekataa kuunga mkono azimio la baraza la usalama ambalo limetoa pendekezo la kuishutumu Israel kutokana na mpango wake kuendelea kujenga makazi ya walowezi katika eneo la Palestina.

Kwenye upigaji kura juu ya azimio hilo, Marekani ilitumia kura yake ya turufu kupinga pendekezo hilo, huku nchi nyingine 14 zikiunga mkono.

 

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Susan Rice amesema kuwa nchi imejiweka kando na azimio hilo ili kuendelea na fursa za kuzileta pande zote kwenye majadiliano juu ya uundaji wa madola mawili.

(SAUTI YA SUSAN RICE)