Skip to main content

Sudan Kusini kuendesha chanjo kwa watoto kukabili polio

Sudan Kusini kuendesha chanjo kwa watoto kukabili polio

Watoto wanaokadiriwa kufikia milioni 3.1 wenye umri wa chini ya miaka 5 katika eneo la Sudan Kusin wanatazamiwa kupatiwa chanjo ya kukabiliana na ugonjwa wa polio.

Kampen ya utoaji chanjo ya kukabili ugonjwa huo inafanyika kwa mashirikiano baina ya serikali ya eneo hilo na mashirika ya umoja wa mataifa, UNICEF na WHO.

 

Chanjo hiyo inayoanza kutolewa February 22, inashabaa ya kutokomeza ugonjwa huo ambao ulilipuka upya tangu April 2008.