Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

KM Ban ataka watawala kujiepusha na kukandamiza maandamano

KM Ban ataka watawala kujiepusha na kukandamiza maandamano

Wakati wimbi la kudai mabadiliko ya kidemokrasia likiendelea kuzikumba nchi za kiarabu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amerejelea wito wake kuwataka watalawa kujizuua kutumia nguvu kama njia ya kuyakandamiza maandamano hayo.

Katika taarifa yake , Ban Ki-moon ameelezea kile alichokiita masikitiko yake kufuatia utumiaji wa nguvu za dola dhidi ya waandamanaji hao ambao wameendelea kumiminika bara barani wakishikiza kufanyika kwa mabadiliko ya uongozi na sera za nchi.

 

Katibu huyo Mkuu amesema kuwa amevunjika moyo kutokana na vitendo vya mabavu ambavyo vinawakumba waandamanaji katika nchi za Bahrain, Libya na Yemen kutoka kwa mamlaka zinazokandamiza maandamano hayo. 

 

Amewataka viongozi katika maeneo husika kuheshimu na kutambua utashi wa wananchi wanaoandamana kwa amani.