Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa tatu kwa ajili ya Darfur waanza

Mkutano wa tatu kwa ajili ya Darfur waanza

Mkutano wa kimataifa kwa ajili ya kusaka njia bora za kusaka amani katika jimbo la Darfur umeanza leo katika mji wa Nyala ulioko kusini wa jimbo hilo.

Mkutano huo ambao ni wa tatu kufanyika unawajumuisha wawakilishi kutoka pande mbalimbali za dunia ikiwemo pia wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na vyombo vingine vya kikanda.

 

Kiongozi wa muungano wa vikosi vya umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID Ibrahim Gambari ni miongoni mwa wajumbe kwenye mkutano huo.

 

Agenda kuu ya mkutano huo ni kusaka njia ya kufikia shabaya ya kupatikana kwa amani ya kudumu kwenye jimbo hilo ambalo limeshuhudia machafuko kwa muda mrefu.