Jitihada zilizopigwa kutimiza lengo la milenia la kulinda mazingira Kenya

Jitihada zilizopigwa kutimiza lengo la milenia la kulinda mazingira Kenya

Ikiwa imesalia miaka mine tuu kabla ya kutimia 2015 muda wa mwisho uliowekwa na viongozi wa dunia kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia, nchi nyingi zinakabiliwa na changamoto za kuyafikia malengo hayo.

Kuna baadhi zimepiga hatua kwenye malengo machache lakini kuna nyingine zinatia mashaka hata ya kufikia asilimia 50 ya malengo yote manane. Moja ya malengo hayo linalopigiwa upatu sana ni kulinda mazingira ambalo ni lengo namba saba.

Kenya kama ilivyo nchi nyingi zinzoendelea hasa za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara hili lengo limekuwa mtihani mkubwa, kwani watu bado wanakata miti, vyanzo vya maji vinaharibiwa na kutoa tisho kwa