Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waanzisha polisi maalumu kuwalinda wanawake Afrika ya kati

UM waanzisha polisi maalumu kuwalinda wanawake Afrika ya kati

Umoja wa Mataifa umeanzisha wataalamu wa usalama ambao watajishughulisha na utoaji wa huduma za usamaria mwema, lakini wakijikita zaidi kwenye maeneo ya kuwalinda wanawake wakimbizi.

Kikosi hicho cha askari polisi ambacho kimepewa mafunzo kupitia kikosi cha kimataifa MINURCART kitawajibika moja kwa moja kutoa ulinzi kwa wakimbizi wa kimataifa mpaka wale wa ndani.

 

Rima Salah ambaye alikuwa mwakilishi msadizi wa ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la afrika ya kati amerejea hivi karibunu mjini New York na kufanya mahojiano na mwandishi wa redio way a Umoja wa Mataifa  Julie Walker . Kwanza alimuuliza changamoto zinazowakabili wanawake kwenye eneo hilo, na ujio wa kikosi hicho cha polisi.

(SAUTI YA RIMA SALAH)