Skip to main content

KM Ban atoa wito kumalizwa kwa mzozo wa Ivory Coast

KM Ban atoa wito kumalizwa kwa mzozo wa Ivory Coast

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametaka kukomeshwa kwa malumbano ya kisiasa nchini Ivory Coast katika wakati ambapo ujumbe kutoka Umoja wa Afrika ukitarajia kuwasili nchini humo kwa shabaya ya kutanzua mzozo wa kisiasa uliosababishwa na matotokeo ya duru ya pili ya uchaguzi.

Ban amezitaka pande zote zinazohitilifiana kwenye mzozo huo, kuweka pembeni mashinikizo yao na kuanza kushirikiana kumaliza mkwamo huo. Alice Kariuki na taarifa kamili:

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)