Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya yaanza kutumia nishati ya mafuta itokanayo na mimea

Kenya yaanza kutumia nishati ya mafuta itokanayo na mimea

Kenya imekuwa nchi ya kwanza katika eneo la Afrika mashariki kuzindua mpango ambao unatumia nishati ya mimea itumikayo kwenye magari hatua ambayo inaweza kuchangia sehemu kubwa kuboresha mazingira.

Nishati hiyo ya disesel itokanayo kwenye mimea tayari imeanza kupatikana kwenye vituo vya kuuzia mafuta na wakati wowote itaanza kuwafikia wateja.

 

Hatua hii inatizamwa ni fursa muhimu ambayo inachangia jitihada za jumuiya za kimataifa za kukabiliana na uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na moshi toka kwenye vyombo vingi vya usafiri.

 

Mpango huo unaungwa mkono na shirika la umoja wa mataifa linalohusika na mazingira UNEP, na kupigwa jeki na mataifa mbalimbali.