Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO, UNICEF yatilia shaka kuzurota kwa sekta za afya Ivory Coast

WHO, UNICEF yatilia shaka kuzurota kwa sekta za afya Ivory Coast

Ripoti kutoka nchini Ivory Coast zinasema kuwa nchi hiyo imekubwa tena na mlipuko wa magonjwa na tayari kuna wasiwasi wa kuanguka kwa misaada ya kibinadamu.

Kwa mujibu wa mashirika ya umoja wa mataifa lile linalohusika na afya WHO na lile la watoto UNICEF kumekuwa na hali ya kuzorota kwenye sekta ya afya kunakochangiwa na kukosekana kwa usalama ambapo baadhi ya maafisa wa afya hushindwa kwenda kwenye vituo vya kazi.

 

Hata hivyo mamlaka zimeanza kujiandaa ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa surua ambao unawaandama watoto wengi. Watoto 500,000 katika eneo la kusin mwa nchi hiyo wanatazamiwa kupatiwa chanjo ya kukabiliana na ugonjwa huo siku chache zijazo.

 

Marixie Mercado ni msemaji wa  UNICEF mjini Geneva: (SAUTI YA MARIXIE MERCADO)

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameonya kuwepo kwa hatari ya kusambaa zaidi kwa mlipuko wa magonjwa kama hakutachukuliwa juhudi za haraka.