Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna maendeleo kwenye kufikia ustawi wa kijamii-ILO

Kuna maendeleo kwenye kufikia ustawi wa kijamii-ILO

Kuna hatua kubwa iliyopigwa kwa mataifa mbalimbali juu ya kuteleza mikakati ya kuboresha ustawi wa haki za kijamii.

Kulingana na ripoti iliyotolewa na shirika la kazi duniani ILO, ambayo imetolewa sambamba na maadhimisho ya siku ha usawa wa kijamii duniani, iliyofanyika hapo jana, hali ya kutambulika kwa haki za binadamu ni miongoni mwa maeneo ambayo yamepiga hatua.

 

Nchi zinazoendelea pia zimepigiwa mfano kwa kuendeleza mageuzi yanayopalilia usalama wa kijamii hatua ambayo ni ishara njema kwa siku za usoni.

 

Akizungumzia hali hiyo, mkuu wa kitengo cha wanawake kwenye Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet, amesema kuwa hata hivyo wanawake bado wanatajwa kuwa ndiyo kubwa kubwa zaidi la watu ambalo bado linaendelea kubaki nyuma kufikiwa na huduma za kijamii.

(SAUTI YA MICHELLE BACHELET)