Skip to main content

Kenya yajiandaa kuwa na mtambo za kinuklia kwa ajili ya matumizi ya nishati

Kenya yajiandaa kuwa na mtambo za kinuklia kwa ajili ya matumizi ya nishati

Kenya imesema kuwa inajiandaa kuanza kuzalisha madini ya nyuklia ili kukidhi mahitaji ya nishati ya umeme ambayo yanaongezeka kila mara.

Taifa hili la Afrika mashariki pamoja na nchi za Ghana na Nigeria linakuwa miongoni mwa nchi 60 zinazoendelea ambazo zimewasilisha maombi yao kwa shirika la Umoja wa Mataifa la nguvu za atomoki kuomba msaada wa kitaalamu ili kuanzisha shughuli hizo.

Matumizi ya nyuklia inatajwa kama njia mbadala ya kuwa na nishati ya uhakika ya umeme. Petar Buselic wa shirika la kimataifa la atomic amezungumza na Winifred Wanjiku Ndubai wa KenGen, shirika la umeme la Kenya, kuhusu mipango ya Kenya kuanza kuzalisha madini ya nyuklia:

(SAUTI YA WINIFRED NDUBAI)