Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiongozi wa UM nchini Kosovo atoa wito kuwepo na uchunguzi kutokana na tuhuma za biashara ya viungu vya binadamu

Kiongozi wa UM nchini Kosovo atoa wito kuwepo na uchunguzi kutokana na tuhuma za biashara ya viungu vya binadamu

Kiongozi wa Umoja wa Mataifa nchini Kosovo jana ametoa wito wa kuwepo na uchunguzi wa haraka kuhusu tuhuma kwamba wafuasi wa kundi la KLA, Kosovo Liberation Army walijihusisha na biashara ya viungu vya binadamu katika mwaka 1999 wakati wa mapambano dhidi ya Waserbia na jeshi la Yugoslavia.