Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa haki za binadamu Haiti apanga kutembelea nchi hiyo

Mjumbe wa haki za binadamu Haiti apanga kutembelea nchi hiyo

Mtaalamu wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya binadamu nchini Haiti Michel Forst, anatazamiwa kuitembelea nchini hiyo kuanzia February 20 kwa ajili ya kutathmini maendeleo yaliyopigwa kwenye maeneo ya uboreshawaji wa haki za binadamu.

Kwenye ziara yake hiyo itakayodumu hadi February 27, Michel atazingatia zaidi juu ya hatua zilizochukuliwa na nchi hiyo kuteleza mpango wa umoja wa mataifa unaohusu mifumo na mageuzi kwenye maeneo ya haki za binadamu

 

Mjumbe huyo pia anatazamiwa kukutana na maafisa wa serikali, maafisa wa mahakama pamoja na wawakilishi wa kikosi cha umoja wa mataifa cha kulinda amani MINUSTAH