Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shirika kubwa la kikanda laahidi kuongeza ushirikiano na UM

Shirika kubwa la kikanda laahidi kuongeza ushirikiano na UM

Shirika kubwa la kikanda la usalama duniani OSCI limeahidi kufanya kazi kwa pamoja na umoja wa mataifa kuhusu maswala ya utulivu Afghanistan ili kuweza kustaawisha nchi hiyo na kupambana na ugaidi pamoja na na kuimarisha ulinzi katka tovuti.

Katika mkutano na Umoja wa Mtaifa, wajumbe OSCE walipongeza nchi ya Lituania katika uongozi wake wa mwaka mmoja wa shirika hilo pamoja na kuzungumzia changamoto zijazo.

Philip Parham, balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa amesititiza umuhimu wa ushirikiano huo

Ufumbuzi wa mgogoro wa Kyrygstan mwezi wa April ulionyesha vyema kiwango cha ushirikiano fika kati ya OSCI , Muungano wa Ulaya na kituo cha Umoja wa Mataifa cha kuzuwia migogoro katika eneo la Asia ya kati.Taasisi hizi zilifanya kazi kwa pamoja katika kusuluhisha mgogoro huo na kurejesha amani na utulivu.

Shirika la OSCI linayo mataifa wananchama 56 Kuanzia Marekani hadi Ulaya na Asia ya kati hadi mipaka ya China.