Navi Pillay ataka kuzingatiwa zaidi kwa ustawi wa wazee

16 Februari 2011

Mkuu wa kamishna ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu Navi Pillay amesisitiza haja ya kuwepo kwa sheria madhubuti kwa ajili ya kulinda ustawi wa watu wazee ambao amesema licha ya kuendelea kuongezeka lakini bado hawajatupiwa jicho.

Hata hivyo amesifu uamuzi uliochukuliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kutenga kitengo maalumu kinachoshughulikia ustawi wa wazee. Kitengo hicho kimeanza kazi rasmi hii leo.

 

Ametaka kitengo hicho kuanza kutafutia ufumbuzi matatizo yanayokabili eneo hilo ikiwemo pamoja na kuangalia sheria za kimataifa na kubuni mbinu nyingine.

 

Kwa upande wake afisa Bwana Craig Mokhiber ambaye ni afisa wa ngazi ya juu kwenye ofisi ya kamishna hiyo amesema kuwa  kukosekana kwa ustawi bora kwa watu wazee ni changamoto kubwa inayokabili eneo la haki za binadamu.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud