Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Navi Pillay ataka kuzingatiwa zaidi kwa ustawi wa wazee

Navi Pillay ataka kuzingatiwa zaidi kwa ustawi wa wazee

Mkuu wa kamishna ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu Navi Pillay amesisitiza

haja ya kuwepo kwa sheria madhubuti kwa ajili ya kulinda ustawi wa watu wazee

ambao amesema licha ya kuendelea kuongezeka lakini bado hawajatupiwa jicho.

Hata hivyo amesifu uamuzi uliochukuliwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kutenga kitengo maalumu kinachoshughulikia ustawi wa wazee. Kitengo hicho kimeanza kazi rasmi hii leo.

 

Ametaka kitengo hicho kuanza kutafutia ufumbuzi matatizo yanayokabili eneo hilo ikiwemo pamoja na kuangalia sheria za kimataifa na kubuni mbinu nyingine.

 

Kwa upande wake afisa Bwana Craig Mokhiber ambaye ni afisa wa ngazi ya juu kwenye ofisi ya kamishna hiyo amesema kuwa  kukosekana kwa ustawi bora kwa watu wazee ni changamoto kubwa inayokabili eneo la haki za binadamu.