Nchi nyingi za Asia-Pacific bado zina sheria kandamizi kwa watu wenye HIV

16 Februari 2011

Nchi nyingi zilizoko katika eneo la Asia-Pacific zimetajwa kwamba bado zimeendeleea kukumbatia sheria ambazo zinawanyima haki watu wanaoishi na virusi vya HIV na wakati huo huo hazijatoa zingatio la kuwalinda wale ambao wapo hatarini kuingia kwenye maambukizi hayo.

Ili kusaka majibu ya kuondosha vikwazo hivyo, makundi ya wataalamu kutoka sehemu mbalimbali wanakutana huko Bangkok kuanzia February 17 kujadilia mikakati na mbinu zinazopaswa kuchukuliwa ili kuzifanyia mageuzi sheria hizo.

 

Chini ya Kamishna maalumu inayohusika na marekebisho ya sheria zinazokwaza juhudi za kukabili maambukizi ya HIV,  wataalamu hao kutoka nchi 22 wanatazamia kujadili mikakati inayoweza uchukuliwa ili kuondosha hali hiyo.

 

Alice Kariuki na taarifa kamili :

 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter