Skip to main content

Umoja wa Mataifa kutuma ujumbe Misiri

Umoja wa Mataifa kutuma ujumbe Misiri

Umoja wa Mataifa umesema kuwa utatuma wataalamu wake nchini Misri kutathmini

hali jumla ya haki za binadamu na wakati huo huo kutafuta upenyo wa kushirikiana

na viongozi wapya kwa ajili ya kuboresha na kulinda haki za binadamu.

Umoja huo wa Mataifa umesema kuwa wakati huu ambapo taifa hilo limeingia kwenye enzi mpya ya demokrasia, lazima kuhakikisha kwamba haki na matwaka ya kila mwananchi yanatiliwa kipaumbele pasipo kuvunja uhuru na haki za binadamu.

 

Umetaka mamlaka zilizopo madarakani kwenye kipindi cha mpito kufungua masikio ili kusikiliza na kuheshimu matakwa ya wananchi.

 

Timu hiyo ya wataalamu wa umoja wa mataifa nchini Misri itaongozwa na Anders Kompass.

(SAUTI YA KOMPASS)