Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji haramu kutoka Misri waanza kuwasili Sicily

Wahamiaji haramu kutoka Misri waanza kuwasili Sicily

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji limesema kuwa zaidi ya

wahamiaji haramu 100 wanaosadikika kutoka Misri wameingia katika eneo la Sicily

lililoko kusini mashariki mwa Italy, wakitumia usafiri wa boti.

Maafisa kwenye eneo hilo wamesema kuwa wamekamati boti nyingine iliyokuwa imebeba wahamiaji 60, iliyotia nanga karibu na kisiwa cha Ragusa. Haijajulikana mara moja wahamiaji hao wametokea maeneo gani ya Misri lakini inadhaniwa kuwa ni

katika mji wa Alexandria.

 

Timu kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wahamiaji IOM, imepanga kukutana na wahamiaji hao kwa shabaya ya kujadilia mambo kadhaa.

 

Wakati huo huo wahamiaji kutoka Tunisia waliowasili kwenye kisiwa cha Lampedusa

mwishoni mwa wiki, wameanza kupatiwa hifadhi kwenye vituo kadhaa nchini Italia