Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay aitaka Bahrain kuheshimu uhuru wa watu kuandamana.

Pillay aitaka Bahrain kuheshimu uhuru wa watu kuandamana.

Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za binadamu Navi Pillay

ameelezea masikitiko yake kwa utawala wa Bahrain ambao amedai umekwenda mbali

mno kwa kutumia nguvu za dola ili kudhibiti maandamano ya wananchi ambao

wamechoshwa na mwenendo wa serikali yao

Vikosi vya askari ambavyo vimetawanywa bara barani kudhibiti maandamano hayo vinadaiwa kuuwa waandamanaji wa wili.

 

Bi Pillay amesema serikali ya Bahrain inapaswa kuheshimu uhuru wa wananchi kuaandamani na akaiitaka pia kujiepusha na utumiaji mbaya wa nguvu za dola.

 

Kamishna huyo ambaye aliitembelea Bahrain mwezi April mwaka jana amesema kuwa ofisi yake inajaribu kufungua meza ya majadiliano na serikali kwa lengo la kupanua uwigo wa shughuli za kisiasa ambazo kwa sasa zipigwa marafuku.