Bei ya chakula yaendelea kupanda duniani-Benki ya Dunia
Ripoti moja iliyotolewa na Benki ya Dunia inaonyesha kuwepo kwa ongezeko kubwa
la bei ya chakula kwa nchi zinazoendelea, hatua ambayo inazusha hali ya wasiwasi
kwa mamilioni ya watu ambao hali zao ni za kipato cha chini.
Ongezeko hilo la bei lililoanza tangu june mwaka jana na kuendelea kupanda hadi sasa limesababisha zaidi ya watu milioni 44 kuangukia kwenye umaskini.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa wakati maafisa wa ngazi za juu wa benki hiyo wakijiandaa kwa mkutano mhimu huko Paris, ongezeko hilo la kiwango 15 asilimia limeanza kukaribia kile kiwango ilichojitokeza mwaka 2008 wakati dunia ilipokumbwa na mtikisiko wa uchumi.
Viongozi wa benki hiyo ya dunia wanaokutana huo Paris wanatazamia kutilia uzito
ongezeko hilo la bei