Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatilia shaka wakimbizi wanaoingia Italia

UNHCR yatilia shaka wakimbizi wanaoingia Italia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR imesema hali mbaya ya

kisiasa inayoandama maeneo ya Kaskazini mwa afrika na mashariki ya kati inaweza

kuchangia pakubwa kuwepo kwa ongezeko la wahamiaji wanakimbilia nchi za ulaya

kupitia bahari ya Mediterranean.

Shirika hilo pia limeonyesha wasiwasi wake juu ya kuwepo kwa ongezeko la makundi yanayoendesha biashara za magendo ambao huwahadaa wahamiaji kwa lengo la kujinufaisha wenyewe

Msemaji wa UNHCR Melissa Fleming amesema kuwa kundi kubwa la wahamiaji kutoka Tunisia wamewasili katika kisiwa cha Lampedusa kilichopo pembezoni mwa Italia.

(SAUTI YA MELISSA FLEMING)

Mashirika ya kutoa misaada yametoa wito wa kuheshimiwa kwa haki za wahamiaji hao hata kwamba hati zao za kupewa ukimbizi bado hazitolewa.