Taasisi za kimataifa zimeshindwa kuwalinda waandishi wa habari:CPJ

15 Februari 2011

Taasisi za kimataifa ambazo zinawajibika kulinda uhuru wa vyombo vya habari zimelaumiwa kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake huku ulimwengu ukishuhudia waandishi wa habari wakiendelea kukabiliwa na hali za vitisho, kuwekwa magerezani na wengine kuuwawa.

Taarifa iliyotolewa na kamati ya kulinda waandishi wa habari CPJ imesema kuwa waandishi wa habari duniani kote wameendelea kushuhudia mazingira magumu ya ufanyaji kazi na huku wengine wakipoteza maisha kutokana na uzembe wa mamlaka zinazohusika kushindwa kuwajibika.

Mkurugenzi wa mtendaji wa kamati hiyo Bwana Joel Simon amesema kuwa wakati sheria za kimataifa zinatambua uhalali wa kuwepo uhuru wa kujieleza lakini katika hali ya kushangaza matunda ya sheria hiyo inawaweka kando waandishi wa habari ambao mara zote wanakabiliwa na hali ngumu.

 

Kamati hiyo imeutaja Umoja wa Afrika kuwa ni miongoni mwa taasisi za kimataifa

ambazo zimeshindwa kusimamia vyema ulinzi wa waandishi wa habari

 

==

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter