Skip to main content

UNHCR yandaa kambi nyingine kuwahifadhi wakimbizi wa ndani wa Ivory Coast

UNHCR yandaa kambi nyingine kuwahifadhi wakimbizi wa ndani wa Ivory Coast

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeanza operesheni ya

kusafisha kambi mpya iliyoko katika eneo la magharibi wa Ivory Coast ambako

kumeripotiwa kukumbwa na uhaba wa makazi.

Hatua hiyo huenda ikasaidia kupunguza hali ya wasiwasi inayowakabili wakimbizi wa ndani ambao wako hatarini kukosa sehemu za kujihifadhi.

 

Kambi hiyo mpya iliyoko karibu na mji wa Duékoué inatazamiwa kuwa na uwezo wa kuwahifadhi watu 6,000 hatua ambayo itapunguza msongamano uliopo kwenye kambi moja ya inayoratibiwa na wanakatoliki.

 

Hata hivyi shirika hilo la kuhudumia wakimbizi bado linaendelea kujipiga kufua kusaka maeneo mengine zaidi kwa ajili ya kuwahifadhi wakimbizi wa ndani kufuatia mzozo uliosababishwa na uchaguzi uliopita.